Jana usiku nilisikia mazungumzo haya kutoka kituo kimoja cha redio fm,
MTANGAZAJI: Asante kwa kutupigia simu umepata bahati ya kuingia kwenye shindano letu la zawadi kubwa ya mwaka huu, uko tayari?
MSIKILIZAJI: Niko tayari
MTANGAZAJI: Swali lenyewe ni la hesabu
MSIKILIZAJI: Mimi mwenyewe mhasibu wa muda mrefu
MTANGAZAJI: Ukitoa jibu sahihi kwa swali hili utapata zawadi yetu nono ya kutembelea soko ambalo ni chanzo cha ugonjwa wa Korona huko Wuhan China, pia kutembelea hospitali mbalimbali huko Marekani kuona juhudi zinazofanywa katika kutibu Korona. Hii ni kampeni ya kituo chetu ya kuhamasisha kujilinda na Korona. Sasa swali….2 +2 ni ngapi?
MSIKILIZAJI: Saba
Categories: Daily Kiswahili Joke