Mapenzi ya Kibongo ni ya aina yake duniani, hivyo nimeona leo nitoe somo ili kuwasaidia mayanki namna ya kuishi kwa furaha katika mapenzi ya Kibongo. Kwanza mapenzi ya Kibongo hayashughuliki na mambo madogomadogo ya kifala kama eti kupeana maua au eti kutembea beach mmeshikana mikono, hizo ishu ni za kwenye sinema tu au labda Ulaya. Hapa watu wako bize wana hangaika na maisha. Wapenzi wa kibongo wa ukweli huwa hawahangaiki kuelezana eti I love you au nakupenda sana , aaa wapi, mdada akiwa na mapenzi ya ukweli utaona anampikia mpenzi wake chakula cha ukweli, jamaa anapokula msosi anajua kuwa kweli huyu mdada ananipenda, hapo hata kama amewakaribisha mabest wake, utasikia ‘Aise huyu demu anakupenda sana kakupikia chakula kitamu hivi’. Katika mapenzi ya Kibongo bili zote mwanaume lazima ulipe. Mkiwa mmekaa baa mmeshakula na kunywa sana hata kama mwanaume unaona mdada kaanza kushika pochi kama vile anataka kulipa jua ni geresha tu, anajua unampenda hivyo utalipa tu. Hata wale wadada waliowahi kuishi Ulaya wanajua system ya Bongo ni mwanaume kulipa. Katika mapenzi ya ukweli ya Kibongo, mdada hata amkute bwana wake na binti mwingine, hata kama wamekaa kihasara yeye huuchuna, tena anafanya kama hujaona chochote, hii itamfanya jamaa ajue mupenzi anampenda sana. Mapenzi ya Kibongo yana mipaka, mdada huruhusiwi kukutwa amekaa kihasara na mkaka. Ili mwanaume wa Kibongo aonyeshe ana mpenda sana mpenzi wake wivu huwa muhimu, mwanaume yoyote, hata kama ndugu marufuku kumsalimu au kutuma mesej au kuchat kwenye simu, hasa giza likianza kuingia. Jambo lingine muhimu katika mapenzi ya Kibongo, mwanaume wa Kibongo marufuku jikoni, kwa sababu mdada anakupenda hata ukirudi saa kumi za usiku na unamkuta ana malaria kali, lazima ajikongoje aingie jikoni, mwanaume ukikosea tu uanze kuingia jikoni kupika ujue umeanzisha mtindo utakaokukosti akipona atadai uendelee kupika na kuosha vyombo na kadhalika. Chunga sana
Categories: Daily Kiswahili Joke