KILA NINACHOOTA KINAKUWA KWEEE, KINAKUWA KWELI


Jamaa yetu alikuwa mahakamani kashtakiwa kwa kosa la mauaji. Akaruhusiwa kuanza kujitetea;
MANGI SAKARIA: Mheshimwa mi ninatatiso kubwa, kila nikiota ndoto inakuwa kwee.. inakuwa kweli. Niliota mke wangu kasaa mapacha kweli akasaa mapaa…mapacha. Nikaota duka langu wamefunja, kweli wesi wakaja wakafuu..wakafunja. Mwesi uliopita sinikaota kari yangu mpya imeungua, siku mbili badae si ikaungua. Sasa nimelasimika kumuua huyu jamaa si usiku niliota ananibaka, inkekuwa wewe mheshimiwa ungekubali kubakwa?

Categories: Daily Kiswahili Joke

Leave a comment