AMRI KUMI ZA MPIRA ENZI ZETU


Pamoja na sheria  17 za soka za FIFA kuwepo, enzi za utoto kulikuweko na sheria za soka ambazo ndizo zilizokuwa zinatambuliwa
1.     Mwenye mpira ndie anaeamua nani atacheza.
2.     Mtoto bonge ndie golikipa
3.     Wachezaji wazuri ndio wanaochaguliwa kwanza
4.     Kukiwa na penati ruksa kubadilisha kipa
5.     Ukipiga mpira kwa nguvu au kwa mandochi mwenye mpira ana ruksa ya kukuonya au kukukataza usicheze
6.     Usipochagia hela ya kujaza upepo mpira utapigwa marufuku kucheza
7.     Hakuna marefa wala malainzmeni, na mpira unachezwa mpaka kuzunguka goli
8.     Kumkaba mwenye mpira faulo
9.     Ukitoboa mpira unalipa
10. Mwenye mpira akikasirika au akiumia au akiitwa na mama yake ndio mwisho wa mechi

Categories: Daily Kiswahili Joke

1 reply

  1. Aisee asante sana san kumbe wewe ni mwandishi mzuri na kweli umenipa moyo wa mimi pia kuandika machache as one of prevelage nikiwa naishii Dar tangu miaka ya 50

    Like

Leave a comment