UNAWAKUMBUKA SUNBURST?


Hawa ndio Sunburst bendi iliyofanya vizuri sana mwanzoni mwa miaka ya 70,mwaka 1973 ikashinda mashindano ya Bendi Bora Dar es Salaam na kuwa ya kwanza. Toka kushoto Toby John Ejuama (saxophone) huyu alikuwa Mnaijeria kutoka Biafra, kama mnakumbuka Tanzania tulimuunga mkono  Ojukwu.!!!! Ejuama alipigia hata bendi ya NUTA Jazz Band enzi hizo. Anaefuata ni Flory mpiga gitaa aliyekuwaMkongo, kisha mkongwe Johnny Rocks kwenye (drums), huyu alikuwa pia anapiga na George Di Souza pale Margot.  James Mpungo (lead vocals) kijana wa Mbeya ambaye hatimae alijiunga na Mangelepa. Anafuatia Kassim Rajabu Magati (organ/lead vocals, kwenye gitaa la bezi ni Bashir Idd Fahani. 

Kutoka kwenye magazeti, picha za washindi watatu wa mwanzo wa mashindano ya Beni Bora Tanzania. Ya kwanza ilikuwa Sunburst, ya pili Tonics na ya tatu SafariTrippers

Leave a comment