BURIANI PADRI YORDA RIP


Padre Giovanni Giorda (RIP)

Padre Giovanni Giorda (IMC) maarufu kwa jina la Padri Yolda amefariki leo mnamo saa 09:40 katika Kituo cha Afya cha Mtakatifu Teresia wa Mtoto Yesu, Wenda. Ni siku chache tu zilizopita niliwahadithia humu jinsi alivyonikamata nikiwa nimetoroka kwa bibi, Msombwe nikitaka kuelekea mjini, ilikuwa mwaka 1959. Mara ya mwisho nimekutana na Padri Yolda ilikuwa tarehe 10 June 2020, nilipoenda kumtembelea pale Tosamaganga, alikuwa mwenye afya njema na kuniambia kuwa sasa ana miaka 93. Akanipa zawadi ya picha kadhaa na kama kawaida akanipa baraka. Najiona kama alikuwa ananiaga. Historia ya Padri Yolda na Iringa inaanza tarehe 9 Desemba 1952 alipoondoka Venice Italia na kuja Tanganyika. Desemaba 24 1952 alifika Dar es salaam na kuondoka siku hiyohiyo kuelekea Tosamaganga, siku chache baada ya hapo alielekea Misheni ya Malangali alikokaa mpaka pasaka ya mwaka 1953. Kwa miezi kadhaa alihamia Rujewa na mwaka 1954 alihamia Tosamaganga alikotulia mpaka mwaka 1965 akiwa mwalimu wa seminari. Mwaka 1965 mpaka 1969 akawa Paroko wa Kilolo, kisha kati ya mwaka 1970 hadi 1980 alikuwa Paroko wa Tosamaganga, akahamishiwa Chosi alikokaa kati ya mwaka 1981 mpaka 988, na mwaka 1989 akarudi tena kuwa Paroko wa tosamaganga hadi mwaka 2007, baada ya hapo ameendelea kuwa Padri hapo Tosamaganga mpaka mauti yake, Misa ya mazishi ya Padre Yolda yatakuwa ijumaa 14/08/2020, saa 4 asubuhi, parokiani Tosamaganga. Pumziko la MIlele umpe EE Bwana na Mwanga wa Milele umuangazie Amina

Categories: Iringa, Uncategorized

Leave a comment