SALIM DHARAMSI AFARIKI CANADA


Katika makala yangu iliyokuwa na kichwa cha habari LEO NIMEKUMBUKA MJI WA IRINGA NILIPOKUWA MTOTO sehemu ya 20 niliandika kuhusu jirani yangu ambaye tulikuwa nae miaka hiyo 1966 na 1967, ambaye baba yake alikuwa na gari limeandikwa LOFA HUYO ANAKUJA na nyuma limeandikwa LOFA HUYO ANAKWENDA. Kwa pamoja tulianzisha library ya kitoto ambayo tulijaza zaidi comics. Kwa masikitiko makubwa nimepata taarifa kuwa Salim Dharamsi amefariki saa chache zilizopita katika mji wa Edmonton huko Canada. Mungu amlaze pema rafiki, jirani na classmate wangu pale Aga Khan Primary School.

Salim Dharamsi wa kwanza kulia RIP

Categories: Iringa

Leave a comment