NIMEAMKA TENA
BAADA YA KIMYA KIREFU NIMEAMKA TENA
BAADA YA KIMYA KIREFU NIMEAMKA TENA
Kwa wale walionaza kufatilia mikasa yangu tangu mwanzo watakumbuka kuwa nilianza kumpenda ‘mchumba’ wa kwanza wakati nikiwa aidha nursery au darasa la kwanza. Mchumba wangu huyu alikuwa mwanafunzi pale Iringa […]
Mji wa Iringa ni mji ambao ni wa watu mchanganyiko kihistoria. Tofauti na historia za miji mingi Tanzania, mji wa Iringa kwanza haukuanzishwa na kabila moja, ni mji wenye historia ya kuchangamsha ambayo ingeweza kutengeneza filamu yenye mvuto mkubwa. Jina la kwanza la mji huu lilikuwa Neu Iringa, likimananisha Iringa […]
BAADA ya bendi kongwe ya Highland Stars kusambaratika mwishoni mwa miaka ya 60, Iringa haikuwa tena na bendi yoyote ya maana, mpaka ilipokuja kuzaliwa bendi ya shule ya Mkwawa, bendi […]
Kama kawaida ya watoto wote duniani, watoto wa Iringa tulikuwa na michezo mingi sana, mingine ya salama mingine hatari kabisa. Wakati tukiwa wadogo hatujui hili wala lile tulicheza sana mchezo […]
Muziki wa soul ulianza kuingia Iringa mwaka 1968 hivi. Nilianza kusikia santuri za muziki wa soul nyumbani kwa rafiki yangu John Silva. Baba yake John Silva ndie aliyekuwa Fundi Mkuu […]
Mke alikwenda kulalamika kwa mumewe kuwa kuna jamaa mgeni jirani kamtukana kuwa ana mdomo kama tairi la trekta. Mume akapandisha na kuapa kutoa adhabu kali sana atakapokutana na huyo mshenzi. […]
NILIPOKUWA na umri wa miaka mitano hivi tulisindikizana na baba kwenye duka la Mhindi mmoja alikuwa akiitwa Fateharis, katika duka lake pia kulikuwa kukiuzwa vitu vya kuchezea watoto, lakini kilichonikaa […]
KUMBUKUMBU za waalimu wa sekondari nyingi, nianze na Mr Jiran, huyu alikuwa mwalimu Mhindi, aliyekuwa na tabia ya kikohozi na kutema mate hata katikati ya kipindi, alikuwa mwalimu mzuri sana […]
Katika makala hizi si mara nyingi nimetaja wasichana, nilipokuwa mdogo wasichana walikuwa na yao na wavulana na yetu. Ila naweza kukumbuka baadhi ya mambo yenye kumbukumbu yaliyojitokeza yaliyohusu wasichana. Jambo […]