TUKUMBUSHANE BENDI ZA VIJANA ZA DAR ES SALAAM MIAKA YA 60


THE TONICS hapa wakiwa kwenye onyesho Arusha

Siku moja niliuliza swali hili……Katika miaka ya 60 hadi katikati ya 70 kulikuwa na bendi nyingi za vijana ambazo unaweza kulinganisha na wanamuziki wa sasa wanaojulikana kama kizazi kipya. Katika jiji la Dar es Salaam, kulikuweko na bendi nyingi kama vile The Sparks, The Comets, The Flames, The Jets, Crimson Rage, The Lovebugs, Trippers Imagination, Safari Trippers, Afro 70. je unakumbuka nyingine ?Majibu……………………  Patrick Tsere said…Yeah kulikuwa na Flaming Stars wengi wao wakiwa wanafunzi wa Minaki miongoni mwao akiwemo Michael Mhuto, Cuthbert Sabuni na mdogo wake John Sabuni, Peter Kondowe (Peko). Hao waliwaka sana mwaka 1966 to 1968. Wimbo wao mmoja ninaokumbuka ni “Mpenzi Maria sisahau x2 Hata nyota nazo, pia mbalamwezi haziwezi kusahau Maria. Usikuu huwa nalia usiku huu huwa naota Maaamaria”. Baadaye wakaenda Mombasa and then they split.

Walikuwepo Hot Five ambayo ilikuwa kali sana miaka hiyo ya 1966 hadi 1969 ilipovunjika ikazaliwa Sparks na Tonics. Ilipokuwa the Hot 5 kiongozi wao alikuwa Michael Jackson na akina Jerry Mwakipesile na Lameck Ubwe. Kwenye drums alikuwa Adam Salumu aka Addy Sally. Ubwe alibakia na Sparks na akina Jackson na Sweet Francis na mdogo wake Green Jackson wakaanzisha Tonics ambayo ilifanya makao yake Arusha wakipiga muziki CAMEO Bar karibu na Msikiti mkuu wa arusha.

When I was in Zambia from 1984 to 1996 nilikutana na Michael Jackson akiwa kwao alikuwa ameugua kichaa wa kuzurura jijini Lusaka amebeba makopo na usingeweza kuamini kwamba ndiye yule aliekuwa star. It was a sad scene I must say.

Kipindi hicho wengine walikuwa the Rifters chini ya Adam Kinguyi, Kijana wa Ilala.

Na hao uliowataja. Of course walikuwepo wakongo kama akina Pascal Onema wakipiga New Palace Hotel ambayo sasa ni Mbowe. Akina Papa Micky na Nova Success. Freddy Supreme (Ndala Kasheba) na Fauvete
  Anonymous said…Kuna bendi ya BAR KEYS ya upanga (kama sijakosea ni 4 flats upanga)sikumbuki wapigaji nilikuwa mdogo sana mpaka leo kuna instumental lao naweza kulipiga kwenye kinanda
  Anonymous said…Brian Shaka and the Oshekas walikuwa Mtaa wa Undali, Upanga.  Anonymous said…Napenda kuwakumbusha groupe moja ya vijana wa Kigoa iliyokuwa ikiburudisha Kilimanjaro Hotel,George De Souza pia kundi lingine ambalo lilitamba sana na nikiwa mpenzi wao,The Sunburst.Mengine mengi tutakumbushana siku za mbele.

Anon said….. Umetaja akina Sabuni ni muhimu usimsahau Raphael Sabuni ambae mara ya mwisho nilimuona live akiwa na STC jazz, wakiwa na Marijani Rajab, na nyimbo zao kama , Ulikuwa usiku wa manane, Rafiki si mtu mwema. 
Top Life Bar Kinondoni bado ni bar, ukiangalia unashangaa kuwa palikuwa pakubwa kiasi cha bendi kupafanya ndo mahala pake, nadhani utakumbuka wimbo wa Papa Micky akisifu Top Life Bar Kinondoni
Anon said……..

Umeisahau kuitaja The Barlock chini ya uongozi wa ndugu wawili Magoa George na Robin Menderez ambao walikuwako New Africa Hotel ambao pia Muhuto aliipitia na kama sitakosea ni kuwa mwanamuziki kijana Huruka (Hucky Dude) Saidi huyu alikuwa nao hawa Sparks, mtafute atakupa story nyumba ya vizuri ambaye ni ushidi hai pia. Yeye ni hazina ya muziki fanya bidii umtafute nadhani bado anakaa Tandika,  kwani nakumbuka alitoroka na Adamu Kingui kwenda Mombasa akiwa bado mwanafunzi sikupi histori ila mtafute uchambuwe mtama naye. Halafu pia ungeulizia watu ambao labda bado wapo hai walioikumbuka Les Strippers ambayo makazi yetu yalikuwa mtaa wa Somali na. 58 kwa binti Omari Nona huyu bibi kesha kufa sasa. Kwani mara ya mwisho nilipokuwa kule miaka minne iliyopita pameuzwa ama kujengwa kisasa

HAYA TUONGEZE KUMBUKUMBU HAPO CHINI WAHENGA …………………

3 replies

  1. Walikuwepo the Heroes wakina Ebby Sykes na Captain Mike.
    Pale Simba grill walikuwepo the Revolutions wakiwa na Melvin
    Brian alikuwa na bendi yake ikiitwa the Pirates
    Of course the Groove Makers bendi ya Sancho Mabeans, Albert Lukindo the Jengos na Habib Jeff kwenye Drums
    Ni lazima tumkumbuke mdogo wake A Babu
    Na Omari Dean Air Bantu nk

    Like

Leave a reply to Cyril Cancel reply