MNAO WAONA WAZEE NAO WALIKUWA VIJANA



KATI YA MWAKA 1966 NA 1973, Ungetembelea miji mingi mikubwa siku za Jumapili, ungekuta vijana waki enjoy kitu kilichokuwa kikiitwa Buggy. Buggy lilikuwa dansi la vijana lililokuwa likianza muda wasaa 7 au nane na kuisha saa kumi na mbili jioni. Ilikuwa marufuku wanafunzi kukutwa kwenye madansa ya usiku hata kama uko sekondari. Hivyo bendi za vijana wengi wakiwa wanafunzi ndizo zilizokuwa zikitamba muda huu. Muziki katika madansa haya ulikuwa zaidi muziki kutoka nchi a magharibi hasa Uingereza na Marekani. Nyimbo za Otis Redding, Sam Cooke, Kipofu Clarence Carter, Wilson Pickett , James Brown,Sam and Dave, Isaac Hayes  na wanamuziki wengine wa muziki wa soul ndizo zilisikika na kuchezwa. Pichani ni mavazi ya enzi hizo?  Si muda mrefu mavazi kama haya yalipigwa marufuku kuwa ni mavazi ya kihuni. Kuliwekwa posters kila kona zikionyesha mavazi sahihi ya kuvaa. Vijana wa TANU Youth League walikuwa wakitembea na mikasi na kuchana nguo zilizoonekana hazifai. Loh, msione wazee wamenyamaza wana siri nyingi……

1 reply

Leave a reply to David Nderimo Cancel reply