LEO NIMEKUMBUKA MJI WA IRINGA NILIPOKUWA MTOTO sehemu ya 30


Cyclostyle machine

Mwaka 1970 lilianzishwa gazeti la shule lililochapishwa palepale shule kwa kutumia mashine iliyoitwa Cyclostyle Machine. Kabla ya kuanza kuchapisha ililazimika utengeneze stensil ya kazi unayotaka kuchapisha, kisha kazi hii unaiweka kwenye hii mashine na kuweka wino baada ya hapo unaanza kuzungusha mashine na karatasi zinachapishwa, mashine ile unaweza kulinganisha na printer za kisasa zinazotumia umeme.
Waalimu waliteuwa Editorial Board ya gazeti, kisha kukakaribishwa makala kutoka kwa wanafunzi. Pamoja na kuweko katika Editorial Board pia ndie niliyekuwa mchoraji wa vibonzo kwenye gazeti hilo ambalo kwa hisani ya mwana editorial Board mwengine Yahaya Shaaban, ambaye ameweza kuhifadhi nakala za magazeti ya mwaka 70 na 71/72 naziweka baadhi ya kurasa za kitabu hicho humu ndani.

Gazeti la shule
John Kitime mstari wa nyuma wa pili toka kushoto
Kazi za shamba
Katuni na John Kitime

Categories: Iringa

2 replies

Leave a reply to Anonymous Cancel reply