Maisha ya sekondari yalikuwa na mambo mengi. Masomo, michezo, sanaa na kadhalika. Wanafunzi nao walikuwa wa aina mbalimbali, wacheshi, serious guys na wanafunzi wasio na mwelekeo mimi nikiwa mfano mzuri. Mchana baada ya masomo watu walitawanyika kwenda kwenye interest zao. Kulikuwa na clubs za kimasomo kama Mathematics club, Geography Club na kadhalika. Michezo ilikuwa mingi sana. Kwenye ukumbi wa shule kulichezwa table tennis na badminton. Nje kulikuwa uwanja wa soka, netball, hockey, cricket, basketball na volleyball. Pembeni ya uwanja wa soka kulizungushwa tracks za kukimbia. Kulikuweko sehemu ya high jump,long jump, pole vault na michezo mingine ya riadha. Kulikuweko na wanafunzi waliokuwa wazuri sana katika michezo yote hiyo. Katika mashindano na shule nyingine , Aga Khan tulirudi na vikombe vingi. Kwenye timu yetu ya soka tulikuwa na watu mahiri kama Abrahman Shaibu, aliyekuwa na umbo dogo lakini mfungaji mwepesi. Kuna mechi ilifanyika pale Samora adhani Lugalo walikuwa wakishindana na Tosamaganga au Malangali, Abrahmani akiyekuwa anacheza wing ya kushoto akafunga goli kipa akakasirika na kuanza kumfukuza ampige. Nadhani alikuwa akiudhika kwanini kajitu kadogo kafunge kirahisi vile. Nikimtaja Abrahmani nakumbuka kuwa tulikuwa basi moja wakati anahamia Dar es Salaam kuja kuendelea na masomo katika jiji hili. Mimi nilikuwa nakuja Dar es Salaam kupata miwani , tukakaa kiti kimoja akawa ananieleza mipango yake na jinsi atakavyoanza maisha katika shule mpya, ni maelezo ambayo nikiyataja leo yatachekesha sana. Tuliachana KIbaha kwani mimi nilishukia pale ili nifikie kwa mjomba wangu Mzee George Mkwawa aliyekuwa Headmaster wa shule ya sekondari ya Kibaha, pale Kibaha Education Center. Wakati huo mwanafunzi ukishapimwa na kuonekana unahitaji miwani, unapewa warrant ya kusafiria kuja Dar es Salaam na miwani unalipiwa na serikali.
Kati ya wanafunzi waliotoka kanda ya Ziwa alikuweko kipande cha mtu aliyeitwa Mbosoli. Mbosoli alisifika kwa kuingia uwanjani na nguo safi nyeupe na kujitahidi kucheza mechi bila kuchafuka. Golikipa aliyetegemewa alikuwa Iddi Mwa ahewa, ubora wa udakaji wa Iddi ulipanda kiwango kama kulikuwa na wasichana wakimshangilia, basi hapo ata ‘dive’ hata kama mpira unakuja polepole. Bila kumsahau mchezaji mwingine aliyekuja kuwa Mkuu wa Mkoa maarufu Bwana Abass Kandoro, na wenzie akina Charles Chotigunga Mdemu, Hamisi Danda na Bonaventure Mligo. Nisimshahu Mwenyekiti wa sasa wa Yanga bwana Mshindo Msollah ambaye alikuwa kwenye kila mchezo, alikuwa katika timu ya shule ya Hockey, alikuwa machezaji mzuri wa basket ball, volley ball na alikuweko katika timu ya soka ya shule.
Burudani zilikuwa nyingi, pamoja na kwaya kulikuwa na drama Club, na kama nilivyoandika kabla kulikuwa na michezo ya kuigiza ya Emmanuel Mkusa, na pembeni kulikuwa na kikundi cha wanamuziki wapiga magitaa. Hapo tulikuwa John Silva, John Kitime, Idd Mwanahewa, na waimbaji kadhaa. Ilikuwa kwenye kundi hili nilipoiona bangi kwa mara ya kwanza, mwenzetu mmoja liileta ikiwa kwenye kikasha cha viberiti, nakumbuka alivuta akaanza kutuambia eti wote anatuona kama samaki tu. Kichekesho kikubwa ni kuwa kile kikasha cha bangi kilipotea kiajabu, kesho yake jamaa akaja analalamika kuwa tulimuibia bangi yake na usiku alishindwa kulala kwa kukosa bangi!! Sigara zilikuwa marufuku kwa wanafunzi lakini kulikuwa na wavutaji wengi ambao walitumia muda wa kupumzika kuvuti sigara zao chooni. Nilikuwa nashangaa ni raha gani walikuwa wakipata kuvutia bangi chooni.

Kulikuwa jiving iliyopata uhai sana baada ya Ambari Nasibu kujiunga na shule. Ambari alikuwa anajua kuimba, kucheza na kupiga filimbi. Akashirikiana na mpiga filimbi mwingine Shaaban Yahaya kikundi cha jiving kikawa moto mkali. Nakumbuka maneno ya wimbo wao mmoja.
Here we are, Here we are,
Down the Dodoma road
At Lugalo Secondary School,
Here we are.
Hawa jamaa wa jiving na suruali zao nyeusi na mashati meupe na viatu vyeusi ilikuwa burudani kubwa sana. Kila shule ilijitahidi kuwa na kundi la Jiving, kundi la Lugalo lilikuwa ni mchanganyiko wa wasichana na wavulana, na lilikuwa kati ya makundi bora katika shule za sekondari.


Baada ya Headmaster Mr Sheikh kuondoka alikuja headmaster wa kwanza Mwafrika wa shule ya Aga Khan sekondari nae aliitwa Mr Ntemo, kuja kwake pia kuliambatana na kubadilika kwa jina la shule na kuwa Lugalo Secondary. Mr Ntemo pamoja na kuwa mwalimu mkuu alkuwa mwalimu wa Civics, na mwalimu Kikudo, aka Kipili akawa anafundisha Siasa. Mwalimu Kikudo pia alikuwa anafundisha Kiswahili, alipewa jina la Kipili kutokana character mmoja aliyekuweko katika hadithi ya Lila na Fila ambayo mwalimu huyu alikuwa akitusomea>>>>>>>>>>>>itaendeleeeeeaM
Categories: Iringa, Uncategorized
Thank you Isingekuwa Headmaster Ntemo sidhani ningeenda High school Sikumoja aliniita ofisini kwake akasema “wewe Ibrahim una ubongo sharp lakini fikira zako ziko kwa wasichana na michezo Sasa nitakupa wajibu wa kuwa Head Prefect. Mtasaidiana na mwenzio huyo nyumbani yako” Nilipogeuka nikamuona dada Sekela monazite wa Jangwani Street ambako nilikuwa naenda sana kumuona mtu fulani…. Kweli u- head ulnisaidia na pamoja na study buddies Mkusa brothers
Thank you for the memories
LikeLike
GREAT KUMBUKUMBU
LikeLike